Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili NECTA

Tagged: 

  • This topic is empty.
Viewing 1 post (of 1 total)
  • Author
    Posts
  • #3664
    Daad
    Keymaster

    Leo NECTA wametangaza orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili, Waombaji ambao majina yao hayatakuwepo watambue kuwa hawakukidhi vigezo vilivyoainishwa katika tangazo la kazi.

    Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) anapenda kuwataarifu Watumishi wa Umma walioomba nafasi za kuhamia Baraza la Mitihani kwa njia ya usaili kuwa baada ya uchambuzi wa maombi hayo, waombaji waliokidhi vigezo wanatakiwa kuhudhuria usaili utakaofanyika tarehe 17 Oktoba, 2024 na 18 Oktoba, 2024. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:

    • Usaili wa kuandika na vitendo utafanyika tarehe 17 Oktoba, 2024 katika Kituo cha Baraza la Mitihani la Tanzania (Mbezi Wani) kilichopo Mbezi Makonde, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Kila msailiwa atapaswa kufika eneo la usaili saa 1:00 asubuhi.
    • Usaili wa mahojiano ya ana kwa ana kwa watakaofaulu usaili wa kuandika na vitendo utafanyika tarehe 18 Oktoba, 2024 katika Ofisi za Baraza la Mitihani la Tanzania Mikocheni, Eneo la Viwanda, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Kila msailiwa atapaswa kufika eneo la usaili saa 1:00 asubuhi.
    • Msailiwa anapaswa kuwa na Kitambulisho cha Kazi kwa ajili ya utambuzi. Msailiwa ambaye hatakuwa na kitambulisho hataruhusiwa kufanya usaili.
    • Msailiwa anatakiwa kufika na Vyeti Halisi ambavyo ni cheti cha kuzaliwa, Kidato cha IV, Kidato cha VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada, Usajili wa Bodi za Kitaaluma, Leseni na vinginevyo kutegemeana na sifa za Mwombaji. Msailiwa ambaye hatakuwa na vyeti halisi hataruhusiwa kufanya usaili.
    • Msailiwa atawajibika kujigharamia chakula, usafiri, malazi au gharama zozote zitakazojitokeza.
    • Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE au NECTA).

    Kwa tangazo hili Watumishi wa Umma walioomba nafasi za ajira kwa njia ya uhamisho watembelee tovuti ya Baraza la Mitihani la Tanzania https://www.necta.go.tz ili kuona majina ya walioitwa kwenye usaili. Aidha, majina ya watakaofaulu usaili wa kuandika na vitendo yatawekwa kwenye tovuti pia siku ya tarehe 17 Oktoba, 2024 kuanzia saa 12 jioni.

Viewing 1 post (of 1 total)
  • You must be logged in to reply to this topic.